“Darling funga macho nikuambie kitu” Bahati alinishurutisha kwa sauti ya upole. Bila kusita, nilifikicha macho yangu kwa viganja vya mkono nikiwa na hamu ya kujua kilichokuwa chaningoja.
Bahati alikuwa na uzoefu wa kunifanyia utani wa aina hii haswa wakati penzi lilkuwa limemchachawiza. Mara ya mwisho alitumia mbinu hii, ni wakati aliponiletea pete ya dhahabu afisini.
Wakati nilipokuwa nimeziba macho, mawazo mengi yaligongana akilini. “labda ana siri Fulani anataka kunieleza ama ni zawadi anataka kunipa? aaah! Potelea mbali, liwe liwalo!” nilijisemeza moyoni.
Ghafla, Mlipuko mkubwa ulisikika hatua chache. sekunde kadhaa baadaye, nilijipata nimelala kifudifudi ardhini huku shati yangu ikitoja damu. “Mungu wangu! Mungu wangu! ” nilibaki kupiga kite huku nikichirizikwa ovyo na damu utosini.
Nilikazana kulinda nguvu kiasi niliyokuwa nimebaki nayo, macho yangu yalipepesa na kuranda randa ovyo nikitafuta alipokuwa Bahati wangu. Mita chache, niliona mawimbi ya bahari yenye hasira yakifagia ufuo na kubingirisha mwili wa mpenzi wangu kuelekea maji makuu.
Nilijaribu kupiga kamsa angalau kuita usaidizi lakini, maghala ya nguvu mwilini yalikuwa tupu. Nilibaki tuu kutizama bahari ikininyanganya kipenzi changu. Ghafla giza nene ilinijia hata nikapoteza fahamu nisipate kujijua.
********************
“Rashidy……………Mzalendo” sauti dhabiti ilinizindua kutoka ule usingizi mzito. “Naam! Ni mimi!” niliitika kwa utiifu, ungedhani nimeitiwa zawadi.
Mawazo yangu yalikuwa yangali yana randa randa. Kufumba na kufumbua nilijipata katika wodi ya wagonjwa mahututi. Kichwa kilikuwa kizito ungedhani limefungiwa gunia ya chumvi.
Pembezoni mwa kitanda, niliona kibuyu fulani kama kibofu ambayo ilikuwa imeshiba damu hata nikadhani naota. “What am I doing in this hospital?” kimombo kilifufuka kinywani.
“Ukweli ni kwamba, umekuwa katika wodi hii kwa miezi miwili sasa. Hii baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa katika hoteli fulani jijini humu. Habari njema ni kwamba angalu umepata fahamu” jamaa mrefu mwenye surupwenye nyeupe pepepe aliniarifu kwa sauti nyenyekevu.
“Where is my Bahati?” zimwi la kimombo lilivamia usemi wangu tena.
Hata kabla ya kupewa jibu kwa swali hilo, tayari picha za kumbukumbu za Bahati wangu zilikuwa zinapishana akilini. Nilijaribu kuzikusanya picha hizo kujua alivyovalia mara ya mwisho tulipokutana lakini singekumbuka.
“We are very sorry to inform you that your lovely Bahati is no more” maneno yale yalipenyeza akilini kama upanga mkali. Tumboni, ningesikia ngurumo fulani kama radi ambayo iliharibia hata minyoo starehe.
Baadaye, nilishindwa kuhimili uzito wa ujumbe ule hata hewa ikanikatikia. “Haraka! Mlete mtambo ya oxigeni tutampoteza jamaa huyu, hurry up! You bustards” daktari alisikika akiwafokea wauguzi.
ENDELEA KUFUATA HADITHI HII YA KUSISIMUA!!!!!!!!!!
Comments