Dunia iliomboleza, kulala kwa Gwiji
MJ tulimpoteza, vilio kwenye miji
Mauti umetukaza, Na tukutane kwa jaji
Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop
Mauti huna arafa, tutayarishe mapema
Robot densi ilifaa, moon walk ikavuma
Ingawa ulikufa, sifa zitakusakama
Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop
Mahasidi wenye wivu, kakupeleka kizimba
Wakakupa maumivu, bila hatia ukaimba
Umerudi kuwa jivu, kwetu ungali simba
Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop
Mahala pema peponi, Na ilale roho yako
Takulinda kama mboni, zisipotee sifa zako
Sinayo woga usoni, kukupea wewe heko
Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop
Comments