Skip to main content

SIRI ZA CHUO KIKUU CHA DAYSTAR

Njoo unisome kwa makini
S.L.P 927
MACHO PLAZA
Kwa wewe unayenisoma,

Habari za utokako? Naona unahema kweli ukitaka kujua yaliyojiri hivi leo kwenye barua hii. Hee! By the way, ikiwa wataka tuelewane naomba uwache kuniangalia kwa hizo macho za kushiba chuki na dharau.

Kabla nikuendelezee udaku! Tafadhali wacha kuangalia kando kando ukinisoma. Unawafanya wapita njia wanadhani tunawasengenya humu. By the way, usha ambiwa na yeyote hivi leo kwamba watamanisha? Ooooooooooooh! Nisamehe. I mean.... you are fearfully and wonderfully made. Sitaongeza wala sitapunguza.

Niwie radhi siwes kutranslate, please! Mwelezee.. aliye kando yako aje akusaidie.
Kabla nikupatie udaku, natamani niulize swali moja tuu. Nihakikishie kwamba hutanuna! Naogopa lakini heri niulize tuu atleast tusafiane nia. Hivi mbona una blush sana? Kama nimekubamba si uniambie tuu ama uwaite wanafunzi wenzako waje wasome uhondo.

Matawi ya miti naona inapukutika kutokana na upepo mkali unaofagilia kutoka milima ya lukenya. Woishe nishikilie! Naogopa itanipeperusha na huenda nikatua penye maadui wa lugha tamu ya Kiswahili.

Back to business! Nina aibu kubwa kukutangazia habari hii. Aaah! Woga potelea mbali. Je! Umesikia kwamba? hivi majuzi wakora wamevamia hoteli moja kule off kampus na kuiba mali inayokisiwa kuwa ya takriban shilingi elfu tano. Hii inajumlisha vipande kadha za ugali wembe pamoja na sufuria ya “nyama”

Duru za kuaminika zilieleza ukurasa huu kwamba CCTV kamera iliyowekwa kwenye hoteli hiyo ya mabati iliwanasa wakora hao wakitekeleza maovu yao. Majina yashatambuliwa ila sitaki kueneza uvumi. Usimwambie mtu lakini nimewasikia watu wakisema genge hilo sugu lilikuwa kwenye orodha maarufu ya “OCAMPO 600”

Kulingana na mwenye hoteli hiyo, genge hilo lilijitokeza likiwa limejiami na bunduki bandia kabla ya kuamrisha wateja kulala chini. Baadaye walifanikiwa kukutoroka na sufuria moja ambayo walidhani ni ya nyama kumbe ilikuwa yenye maji ya kuosha vyombo pamoja na vipande hivyo vya ugali.

Nishakwambia! Ndo maana nikapewa jina barua na jukumu langu likawa ni kusafirisha ujumbe.

Kumbuka kunisoma kila ijumaa nkupe yaliyojiri katika ulimwengu wa umbea. kuwasiliana nami mtumie bosi wangu ujumbe kupitia kujiuunga na kundi la WAKIDA kwenye mtandao wa FACEBOOK ama msikize kila alhamisi jioni kwenye idhaa ya SHINE FM 103.1 katika kipindi cha KIMBUNGA CHA JIONI.

akhsante kwa wakati wako,

niite Odhiambo Danyell ama ukipenda Rashidy

nimeondoka.....

Comments

my say my take said…
maneno mazuri haya nataajia kuona mengi
tasha said…
i like baby........
nawashkuru warembo kwa kuendelea kutembelea ukurasa huu!

Popular posts from this blog

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

OPERATION TUTETEE WANAUME!!!

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL SEHEMU YA KWANZA: Mzee Matendechere alionekana kuokotwa na usingizi mwepesi wakati akiuguza majeraha ya panga hospitalini. Kisa na maana, adabu ilimhama mkewe hata akaamua kuchukua sheria mkononi na kumpa mumewe kichapo cha mbwa kabla ya kutorokea kusichojulikana. Kichwa chake kilibanwa kwa kilemba cheupe chenye matone ya dam u. Isitoshe, Kwenye shavu la kushoto, palidhihirika jeraha bichi lenye kushonwa kwa uzi. Cha kusikitisha zaidi, Pembezoni mwa kitanda, wangeonekana wapiga picha kutoka vyumba vya habari waking’ang’ana kuchukua picha za kuvutia watazamaji. picha kwa hisani ya http://medievalminds.com Maskini Matendechere alizidiwa na usingizi hata akabakia kukoroma huku akifungua mdomo mithili ya mamba mwenye njaa. “Wow! This seems to be the best shot, I,m loving this” alisikika akisema mmoja wa wapigaji picha tuliyeshuku ni wa asili ya kimarekani. Kweli, vita vya panzi furaha ya kunguru. Wakati haya yakijiri, ndoto ya m...

KUMBU KUMBU ZA MWANA HAWA

MTUNZI: Odhiambo Danyell Manyunyu mepesi ya mvua yangesikika yakikung’uta mabati na kuibua mdundo flani iliozidisha tamaa yangu ya  kuendelea kupanga mbavu kwenye kitanda. Mara, alisikika jogoo mmoja kijijini akiwika kama kuashiria nuru ilikuwa imekubali zamu yake ya mchana. Nilibaki kugaragara kitandani huku mabishano makali yakiendelea akilini kati ya mwili dhaifu na nafsi yangu. Mwili ilisisitiza niendelee kulala huku nafsi ikinisihi niamke. Baada ya kutafakari kuhusu hasara za usingizi niliridhia kuamka. Ghafla, fikra zangu zilielekezwa katika saa kubwa iliyoning'inia ukutani ambayo ilikatiza hali ya unyamafu uliokuwa umetawala chumbani. kuzidisha, chenene fulani aliyekuwa kajificha mvunguni alianza kutoa sauti ya kuudhi. “Aah! Heri tuu niamke” nilijisemeza huku nikijikokota kuelekea kwenye dirisha. Nikichungulia nje, ningeona kunguru wakipigania makombo ya chakula kwenye pipa iliyosimama mkabala na chumba changu. Isitoshe, rukwama kukuu za wazegaz...