Skip to main content

MAPENZI KIZUNGU ZUNGU

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL

Mawimbi makali baharini yalikimbizana na hatimaye kusukuma maji hadi ufukweni. Pembeni, Bahati alionekana ameshika kijiti kirefu mkononi akijaribu kuchora umbo la moyo wa mapenzi kwenye changarawe mbichi huku maji ya bahari yakifuta.

Angani, ndege aina ya korongo na mbayu wayu wangeonekana wakicheza cheza huku tufani kali zikifanya matawi ya minazi ufuoni kupukutika. Nikijistiri juu ya roshani(balcony) katika hoteli ambayo tulikuwa tumekodisha nilisalia kula kwa macho.



Nilibakia kinywa wazi kuona madhari ya kutamanisha jinsi jua ilizama upeoni na kufanya maji ya bahari kupiga rangi ya manjano. mawazoni, nilitawaliwa na picha za harusi yetu jana yake katika ukumbi wa pataneni.

Hatua chache niliona suti yangu ambayo ilikuwa ingali sakafuni baada ya usiku yenye sarakasi si kidogo. Ajabu, marashi yenye uhai aliyopiga Bahati ilikuwa bado imesakama pua yangu.Waliosema harusi ni kilele cha mapenzi hawakukosea hata kidogo.

“Honey…………Rashidy! Rashidy!” Kwa mbali, nilimsikia Bahati wangu akiita. Nilipogeuka nilimwona akiruka huku akirusha mkono kama kunisihi niende alipokuwa.

Nikivalia makubadhi ,suruali fupi ya samawati na shati yenye michoro ya vibonzo na taratibu nikateremka kwenye ngazi ya mbao. badaye nilifuata njia ya nyasi iliyochongwa kando kando kuelekea alipokuwa mpenzi wangu.

Bila kusita alikimbia na kunirukia kwenye mabega huku akizamisha busu moto kwenye shavu langu. Hisiya kweli hazifungiwi mlango………………………endelea kutembelea ukurasa huu ujue yapi yatatokea katika hadithi hii

Comments

Wanja said…
Great stuff.....ama tunacomment in swa?
@Wanja mradi ume eleweka. shukran kwa maoni yako.
annayt said…
this is beautiful. i love it. :)

Popular posts from this blog

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

SIRI ZA “JAM” JIJINI NAIROBI; TOLEO LA PILI

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Jinsi basi lilivyozidi kufukuzia kuelekea mzunguko wa Nyayo stadium, ndivyo ilizidi kuwachilia moshi ya mpingo iliyosokota angani kabla ya kutawanyika. Pale pia, tulimpata polisi wa trafiki mwanamke aliyefungia mshipi wa longi yake kwenye kifua. Amini usiamini, kwa ishara ya mkono alielekeza mkondo wa gari kama jinsi upepo huele ... keza bendera. Pale tulis...imama kwa dakika chache kabla ya msongamano kufunguliwa. Cha kuvutia tamaa ya macho yangu ilikuwa ‘tuk tuk’ fulani ambayo ilipenya penya kati kati ya magari huku ikipiga kelele kama mashine ya kusaga mahindi. Wenzangu wanaiita kule bara POSHOMILL. “We! Boss, ondoa hiyo kabati kwenye barabara” alisikika akishambuliwa na mmoja wa madereva wa matatu. Wanasema muungwana hununa moyoni na wala siyo mashavuni na kwa hivyo Yule dereva wa ‘tuk tuk’ akaridhia kumjibu kwa kimya. Kando na tukio hili, kuna jambo lililotendeka ambalo liliwacha mbavu za kila mtu zikiuma. Niseme nisiseme! Aaaah! ...