MTUNZI: Odhiambo Danyell
Manyunyu mepesi ya mvua yangesikika yakikung’uta mabati na kuibua mdundo flani iliozidisha tamaa yangu ya kuendelea kupanga mbavu kwenye kitanda. Mara, alisikika jogoo mmoja kijijini akiwika kama kuashiria nuru ilikuwa imekubali zamu yake ya mchana.
Nilibaki kugaragara kitandani huku mabishano makali yakiendelea akilini kati ya mwili dhaifu na nafsi yangu. Mwili ilisisitiza niendelee kulala huku nafsi ikinisihi niamke. Baada ya kutafakari kuhusu hasara za usingizi niliridhia kuamka.
Ghafla, fikra zangu zilielekezwa katika saa kubwa iliyoning'inia ukutani ambayo ilikatiza hali ya unyamafu uliokuwa umetawala chumbani. kuzidisha, chenene fulani aliyekuwa kajificha mvunguni alianza kutoa sauti ya kuudhi.
“Aah! Heri tuu niamke” nilijisemeza huku nikijikokota kuelekea kwenye dirisha. Nikichungulia nje, ningeona kunguru wakipigania makombo ya chakula kwenye pipa iliyosimama mkabala na chumba changu. Isitoshe, rukwama kukuu za wazegazega waliosambaza maji kijijini nazo zilisikika zikipita cheke! cheke! cheke!............cheke!. Aha! kumbe ndo ujanja wao wa kuwaita wateja.
“usione nasinzia, unayoyasema nayasikia”
Kama ada, mimi hupenda kuanzisha asubuhi yangu na kipindi moja maaarufu sana redionia. Kwa hivyo, taratibu nilinyosha mkono na kuwasha redio iliyokuwa inazungumza japo kwa udhaifu. "hawa mende wamevamia redio hata ikapata homa" nilijisemeza.
“usione nasinzia, unayoyasema nayasikia” mtangazaji mmoja kwenye kipindi maaarufu cha PAMBAZUKA kwenye idhaa ya SHINE FM alisikika akisema. "hahhaha........haahah! sadfa iliyoje" nilisema huku nikicheka. ungedhani amesikia usemi wangu.
Tuyawache hayo. Akilini, palisongamana mawazo ambayo yalinifanya nijihisi kama mahame ya uhai. Kiwiliwili changu kilijihisi kuvaliwa na unyonge ajabu nisijue la kufanya. "Mashetani haya yataniua leo!" nilitamka. Pembezoni mwa kitanda palisimama chupa nyembamba ya ‘whisky’.
Bila ya kujali lolote, nilimimina chupa ile kabla ya kupiga mswaki angalau kufukuza harufu yake ambayo ingenisaliti kwa mjomba. Tulikuwa tumeishi kwa amani tangu aliponipa hifadhi miaka miwili iliyopita na sikutaka la kutuvunjia uhusiano huu.
Mara moja mvinyo ilijisambaza mwilini hata nikapata utulivu wa ajabu. Ghafla, kisunzi kilinijia na hata nikajiona mfalme mwenye himaya kubwa ajabu. "Ghaddafi! huyo hatoshi mboga!”
Mvinyo ile ilivyozidi kutembea mwilini ndivyo furaha ya ghafla ilinifurika. Maisha peremende! Nilisema huku nikicheka pekee yangu. Katika hali hiyo, maisha ilikuwa sherehe isiyo na kifani.
Krrrr! Krrrrrr! Simu ya rununu kwenye meza ilisikika ikilia.
Rashidy: Halo!.…Hallo!.......... Hallo!
Mwana Hawa: uhali gani mpenzi wangu?
Rashidy: Niko salama tuu ila nimekupeza ajabu.
Mwana Hawa: usijali mpenzi wangu kila kitu ki shwari.
Rashidy: Hamna neno dia.
Mwana Hawa: Mpenzi hebu tega sikio kuna la dharura natamani nikujuze.
Rashidy: kulikoni? Niambie tuu!.
Mwana Hawa: wazazi wangu wamenilazimisha kuenda kusoma uarabuni. Hivi naondoka leo usiku na sioni tukikutana tena Nakusihi unisamehe kwa kukueleza haya dakika ya mwisho.
Rashidy: eti nini? (ghafla simu inakakatika)
Matukio ya aina hii ni nadra sana kutendeka katika maisha ya mwanamume. Na kwa hivyo nilijipata kupandwa na hasira nisijue wa kumwelekezea. Bila ya kujali hili ama lile nilijipata nimeshika chupa tupu ya “whisky” na kuitupa ukutani.
Matukio ya aina hii ni nadra sana kutendeka katika maisha ya mwanamume. Na kwa hivyo nilijipata kupandwa na hasira nisijue wa kumwelekezea. Bila ya kujali hili ama lile nilijipata nimeshika chupa tupu ya “whisky” na kuitupa ukutani.
“Rashidy! Rashidy! Kuna fujo gani humo?” mjomba alisafisha koo kabla ya kupaza sauti akiuliza.
“Samahani mjomba, ni chupa ya soda imeteleza kutoka mezani na kuanguka sakafuni” nilijiami kutumia uwongo.
Tuwache hayo, turudi dunia yangu ya huzunii. Kweli! shida haibishi hodi. haijui maskini wala tajiri, mweupe ama mweusi...............eee! mungu nisaidie.
Maswali yaliyoibuka baada ya simu ile ni mengi ila sikujua pa kupata jibu. Aha! Mungu hamwachi mja wake, nilijisemeza huku nikijifariji.
Nilikumbuka kuna huduma ya okoa jahazi. Simu tayari ilikuwa sikioni nikisubiri kusikia sauti nyororo ya Mwanahawa.
“Sorry the mobile subscriber cannot be reached” hadi wa sasa, ningali nakumbuka majibu hayo niliyopokea baada ya kubaini kwamba alikuwa kazima simu. Lisilo budi hutendwa na kwa hivyo nilijikaza kuokoa wasaa angalau nifike kwao nyumbani kujua mbivu na mbichi.
Champali nilizivaa, kofia ya chepeo ikajistiri kichwani kabla ya kukaza mshipi. Mara moja nilipenya penya kwenye vichochoro vya maji taka nisizuiwe na harufu mbaya iliyokuwa imeshiba hewani na kuchokoza usalama wa pua.
Rashidy! ……….Rashidy nilisikia sauti nyororo ikiniita wakati nilipopita mkahawa wa mabanda wa ‘cool breeze’. Ama kwa hakika sauti ilikuwa ya kuvutia ila sikutaka kusikia lolote ila kujua jinsi ya kumpata Mwanahawa.
Nilipita kona moja, mbili na hata bonde la mwisho ndipo nikampata mbwa mmoja mweusi tititi akitulia chini ya mwembe. Kumbe sikujua ukorofi wake. Mara, alianza kubweka kama ambaye amepokonywa mfupa wake.
"Aah! unatishia nani?" nilimshambulia kwa maneno ungedhani anasikia. Punde, nilianza kukusanya ujasiri wangu na kutembea taratibu hadi nilipomwona akinyemelea kisigino ndipo nikajua mazishi yanukia.
"Aah! unatishia nani?" nilimshambulia kwa maneno ungedhani anasikia. Punde, nilianza kukusanya ujasiri wangu na kutembea taratibu hadi nilipomwona akinyemelea kisigino ndipo nikajua mazishi yanukia.
kando kando nilipitana na kundi moja la watoto waliokuwa wakimshangilia mbwa yule. "saadam! saadam! kamata mtu! kamata mtu!" “kumbe jina la baradhuli yule ni Saadam?” nilijisemeza kimoyomoyo.
Safari ya ajabu
Mimi huyoo! Nilichana mbuga huku mbwa yule gaidi akinifukuzia nyuma wakati akibweka na kumwaga nyute ni kama ameona nyama choma.
Bahati yangu nikapita kwa kasi na kuruka mtaro kubwa ya maji taka ndipo mbwa akaona ujanja wake umekwisha.
Ujanja wa nyani kweli huishia jangwani. "wewe! ningekumaliza leo" nilisema nikijipiga kifua.
Bahati yangu nikapita kwa kasi na kuruka mtaro kubwa ya maji taka ndipo mbwa akaona ujanja wake umekwisha.
Ujanja wa nyani kweli huishia jangwani. "wewe! ningekumaliza leo" nilisema nikijipiga kifua.
Sitasema wakati huo nilikuwa nahema kwa nguvu huku kijasho kikinitiririka njia mbilimbili mashavuni. utacheka na leo labda kesho ni wewe.
Niliwasili pale kwao dakika chache baada ya saa mbili asubuhi. Chini ya kitalu cha miembe kwenye baraza, niliwapata wazee wake wameketi nje ni kama wanajadiliana kuhusu jambo la siri. Kama kijana mnyenyekevu, niliwaamkua kwa heshima kabla ya kuulizia alipokuwa mpambe wangu.
“kijana mbona wahema ni kama unafukuzia mawindo?” aliuliza mzee moja mwenye kipara cha kung’aa aliyevalia kanzu nyeupe. Chini ya viti palisimama glasi za kusheheni mnazi hata nikajua nimefika pa wenzangu.
“Nimefukuzia huku kumtafuta Mwana Hawa. Kuna ujumbe muhimu niko nao kutoka kwa mwalimu” nilijikinga na maswali kwa kudanganya.
“Pole kijana ila ni vizuri nikuarifu Hawa kesha ondoka majogoo kuelekea Nairobi kuabiri ndege ya auarabuni kwa mchumba wake. Nenda kamwambie mwalimu wenu Mwanahawa si wa hapa kijijini tena.”
Siku nyingi nimewalaani wale wa kujitia kitanzi ila sitaficha lolote kufichua kwamba wakati huo nilijihisi gofu tuu lisilo na maana. “mauti njoo unichukue” hayo ndiyo mawazo yaliyovaa.
Taratibu nguvu ilinishuka kabla ya fahamu kunihama. “Ala! Kisirani aina gain hii, kijana amekuja kufia hapa?” alizusha mzee mmoja.
Buriani
Heri niseme nilimpenda kwa dhati, msichana aliyenivumishia sifa pamoja na kuniongezea maadui kutokana na urembo wake.
sijui kama tutawahi kutana tena. nishapata udaku kwamba ni mja mzito. walimwengu kweli hawana imani.
“Kwaheri Mwanahawa, ulinisaliti duniani tukutane na akhera” nilijisemeza moyoni.
Comments