Januari tarehe 23, 2012 Saa iliyotulia wima kwenye kuta ya hema ilifichua kwamba ilibakia dakika chache kabla ya saa nane mchana . Akilini halikunijia wazo kwamba jaji wa mahakama ya Hague Bi Ekaterina Trendafilova alikuwa anasubiriwa kutoa uamuzi wa korti dhidi ya washukiwa sita wa vita vya baada ya uchaguzi. Msimu wa masika tayari ulikuwa umeenda likizo, kiangazi kilikuwa kinatawala na umaarufu wa jua kijijini ungedhihirika kwa jinsi miale yake ilizidi kukausha nchi kavu hata nyufa zikatawala ardhini. kambi ya wakimbizi ya faraja Mara kwa mara, tufani kali za kutoka magharibi zingesikika zikifagilia na kufanya matawi ya miembe kupukutika kabla ya kuchezeshwa angani ovyo ovyo. Nilikuwa nimetulia kwenye mkeka ndani ya hema ndipo nikagutushwa na unyamale uliojiri kwenye kambi ya wakimbizi ya faraja. Mara moja, nikashuku hatari na kuchungulia nje angalau kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa. Nikisimama kwenye mlango ya hema, ningehisi hali isiyo ya kawaida. Upweke ulitawala k...
JAMVI LA BURUDANI,MAARIFA NA USHAURI