Skip to main content

USHUHUDA WA MKIMBIZI

Januari tarehe 23, 2012
Saa iliyotulia wima kwenye kuta ya hema ilifichua kwamba ilibakia dakika chache kabla ya saa nane mchana . Akilini halikunijia wazo kwamba jaji wa mahakama ya Hague Bi Ekaterina Trendafilova alikuwa anasubiriwa kutoa uamuzi wa korti dhidi ya washukiwa sita wa vita vya baada ya uchaguzi.

Msimu wa masika tayari ulikuwa umeenda likizo, kiangazi kilikuwa kinatawala na umaarufu wa jua kijijini ungedhihirika kwa jinsi miale yake ilizidi kukausha nchi kavu hata nyufa zikatawala ardhini.
 kambi ya wakimbizi ya faraja

Mara kwa mara, tufani kali za kutoka magharibi zingesikika zikifagilia na kufanya matawi ya miembe kupukutika kabla ya kuchezeshwa angani ovyo ovyo. Nilikuwa nimetulia kwenye mkeka ndani ya hema ndipo nikagutushwa na unyamale uliojiri kwenye kambi ya wakimbizi ya faraja. Mara moja, nikashuku hatari na kuchungulia nje angalau kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.

Nikisimama kwenye mlango ya hema, ningehisi hali isiyo ya kawaida. Upweke ulitawala kote japo kwa ndege ambao walikuwa katika shughuli ya kujenga viota juu ya miembe. Hii ilikuwa tofauti na hali ya kawaida ambapo kelele za majirani zingevunja tamaa ya mtu kutaka kuonja usingizi wakati wa mchana.

Hata kabla ya mate kunikauka mdomoni, upepo mkali ulifagilia na kupepeta kila kitu ndani ya hema hata nikahofia ingeng’oa hema. “shetani ashindwe!” nilitamka maneno hayo kumkemea ibilisi ambaye tuliambiwa huandamana na upepo ya aina hii na kuletea wanadamu nuksi.

Kabla ya fikra zile kunikauka akilini, nilinyongwa na mate nikikadiria madhara ya upepo ule. Picha za familia yangu nilizozistiri kwenye kioo ziliangushwa na vipande vya kioo vikabaki kutapakaa sakafuni.
Picha hizo zilibeba kumbukumbu ya wazazi wangu pamoja na mandugu zangu mapacha ambao waliuliwa kinyama wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Shetani ashindwe!
Ghafla, milango ya machozi ilijiwachilia huru na nikadondokwa na machozi kama kitoto nisijue la kufanya. Nilijihisi ni kama nimedungwa msumari moto kwenye kidonda mbichi. Maumivu yalinizidi hata wazo likanijia la kujitoa uhai kwani uzito huu ulikuwa umelemea mabega yangu.

Nilijiliwaza nikisemeza moyoni. “heri mimi nimebaki na picha, laa sivyo nisingepata fursa kuona sura zao tena baada ya mkasa ule wa moto.” Kila mara nikisema hivi nilihisi nimefarijika kwani mara ya mwisho kuwaona familia yangu ilikuwa mkesha wa siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu. Singedhani kwamba katili fulani angefikia kauli ya moto nyumba yetu na kuwabadilisha wote kuwa jivu.


Aha! Kilio cha dakika chache kilisaidia kufungua macho ya ubongo wangu ambayo ilikuwa imeziba. Nilishangaa kamasi nyepesi ikinitoka puani hata nikahitimu kuwa zuzu.

“ Ala! Kumbe leo ni siku ya kutolewa kwa uamuzi wa korti ya kimataifa ya Hague kuhusiana na wale wasita wanaoshukiwa kuchochea vita vya baada ya uchaguzi? No wonder! ” nilijisemeza huku nikingata ulimi.

Kama mwenye kupandwa na kichaa nilijizoa kutoa sakafuni na kupanguza machozi kabla ya kufululiza hadi kwenye ukumbi wa burudani wa pataneni pale kijijini. Nilijua ni hapo pekee ndipo nilikuwa na hakikisho la kupata kutizama televisheni. Pale palifurika furi furi hata nzi hangepata mahala pa kutua salama. Nilijaribu kepenya katikati ya umati lakini lo! Ilishindikana.

Bi Ekaterina Trendafilova asoma uamuzi wa korti!!

“Daima dua la kuku halimpati mwewe” nilisema kimoyomoyo. Hayo ndiyo mawazo yaliyorandaranda akilini wakati Bi Ekaterina Trendafilova aliposoma uamuzi wa koti. Nilijua daima mnyonge hana haki na kwa hivyo nilijitayarisha vilivyo kupokea uamuzi nikijua washukiwa hao wangeondolewa mashtaka.


Ghafla, nilikunakuna sikio alipofikia kilele cha uamuzi kuhakikisha nta haingenizuia kupokea ujumbe ule moja kwa moja. Singeruhusu masikio kuokota uvumi wakati kama huo kwani uamuzi huu ungepelekea kudumisha haki kwa wahasiriwa wa vita hivyo almaarufu Post Election Violence. Angalau usiseme sijui kimombo.

Lililofuata ni ujumbe ambao ulifanya magoti yangu kuingia unyonge kwani wawili kati ya washukiwa wasita walitolewa mashtaka na nikabaki kujua wanne waliobaki pia wangeepuka hivyo tuu!
Katika ukumbi huo singejizuia kuona nyuso za wakimbizi wenzangu ambazo zilitawaliwa na mchanganyiko wa hisiya za ghadhabu pamoja na huzuni huku kope za wengine zikionekana kuloa machozi.

Baadaye ilitangazwa kwamba Hussein Ali pamoja na Henry kosgey walikuwa wameondolewa mashtaka kutokana na uchache wa ushahidi. Kwa upande mwingine, Uhuru Kenyatta, William Ruto, Francis Muthuara na Joshua Arap Sang walijipata matatani  wakielekezwa katika mkondo wa pili wa kudhibitisha kesi dhidi yao.

Ajabu, Minongono ilisikika kichinichini na baadaye kutawala wakati wengi wakionesha kutoridhishwa na uamuzi ule. Sekunde chache baadaye, umati ulifumukana na kila mmoja akaelekea kwake. Kila mmoja alivalia sura ya mazishi.

Adhabu ya mlevi
Kwa umbali, mlevi mmoja alisikika akishangilia uamuzi huo akisema wote hawana hatia ni kusingiziwa tuu. “aaaaaaaaa! Porojo tupu. Hata hao wengine watatolewa tuu mashtaka” alisikika akisema.

“Uuuuuuwi! Uuuuuuwi! Nisaidieni! Nisaidieni!” hiyo ndiyo sauti iliyosikika baadaye. Tulipoharakisha kuelekea palipokuwa na kelele hiyo, tulimpata mlevi huyo amepewa kichapo cha mbwa huku damu ikimtiririka ovyo ovyo.
“Ni nini ya maana kabila zetu ama kudumisha umoja baina ya kabila zetu” aliuliza chifu huku umati ukimjibu kwa sura za mashangao!

Comments

Popular posts from this blog

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

OPERATION TUTETEE WANAUME!!!

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL SEHEMU YA KWANZA: Mzee Matendechere alionekana kuokotwa na usingizi mwepesi wakati akiuguza majeraha ya panga hospitalini. Kisa na maana, adabu ilimhama mkewe hata akaamua kuchukua sheria mkononi na kumpa mumewe kichapo cha mbwa kabla ya kutorokea kusichojulikana. Kichwa chake kilibanwa kwa kilemba cheupe chenye matone ya dam u. Isitoshe, Kwenye shavu la kushoto, palidhihirika jeraha bichi lenye kushonwa kwa uzi. Cha kusikitisha zaidi, Pembezoni mwa kitanda, wangeonekana wapiga picha kutoka vyumba vya habari waking’ang’ana kuchukua picha za kuvutia watazamaji. picha kwa hisani ya http://medievalminds.com Maskini Matendechere alizidiwa na usingizi hata akabakia kukoroma huku akifungua mdomo mithili ya mamba mwenye njaa. “Wow! This seems to be the best shot, I,m loving this” alisikika akisema mmoja wa wapigaji picha tuliyeshuku ni wa asili ya kimarekani. Kweli, vita vya panzi furaha ya kunguru. Wakati haya yakijiri, ndoto ya m...

KUMBU KUMBU ZA MWANA HAWA

MTUNZI: Odhiambo Danyell Manyunyu mepesi ya mvua yangesikika yakikung’uta mabati na kuibua mdundo flani iliozidisha tamaa yangu ya  kuendelea kupanga mbavu kwenye kitanda. Mara, alisikika jogoo mmoja kijijini akiwika kama kuashiria nuru ilikuwa imekubali zamu yake ya mchana. Nilibaki kugaragara kitandani huku mabishano makali yakiendelea akilini kati ya mwili dhaifu na nafsi yangu. Mwili ilisisitiza niendelee kulala huku nafsi ikinisihi niamke. Baada ya kutafakari kuhusu hasara za usingizi niliridhia kuamka. Ghafla, fikra zangu zilielekezwa katika saa kubwa iliyoning'inia ukutani ambayo ilikatiza hali ya unyamafu uliokuwa umetawala chumbani. kuzidisha, chenene fulani aliyekuwa kajificha mvunguni alianza kutoa sauti ya kuudhi. “Aah! Heri tuu niamke” nilijisemeza huku nikijikokota kuelekea kwenye dirisha. Nikichungulia nje, ningeona kunguru wakipigania makombo ya chakula kwenye pipa iliyosimama mkabala na chumba changu. Isitoshe, rukwama kukuu za wazegaz...