MTUNZI:ODHIAMBO DANYELL
Dereva wa basi la kampuni ya RWAKEN alijistiri mbele ya usukani na kupiga gari moto wakati tukiondoka katika kitivo cha chuo kikuu cha Daystar yenye makao katika mzunguko wa barabara ya Valley road, Nairobi.
Ilikuwa dakika chache baada ya saa kumi na nusu jioni. Hii ni kumaanisha, wafanyikazi pamoja na wanafunzi wa mchana chuoni tayari walikuwa katika harakati zakufunganya virago na kurejea makwao baada ya panda shuka za mchana.
Vvrrrrrrrrrrrrrm! vvrrrrrrrm! Dereva alipasha gari moto na taratibu basi likaelekezwa nje ya lango kuu. kabla ya kuingia kwenye barabara kuu ya Valley road.
Auuuuuwi! imagine mbele yetu palisimama gari aina ya Range Rover Vogue iliyowachilia moshi nyeupe iliyosokota na kupata hifadhi katika mapua ya basi la RWAKEN. Katika mbuga la wanyama, gari hili linalinganishwa na mfalme Simba kutokana na udhabiti wake. Mashini hii yasifika kwa ulafi wa petroli pamoja na muundo wake wa kutamanisha. Aha! Sasa nimejua kwanini basi ilikuwa inanguruma kama yenye mafua....
Kando na hayo, sisemi nilivutiwa zaidi na rangi yake nyekundu ya kukoza pamoja na ‘rims’ za shaba ukipenda silver na isitoshe magurudumu inchi sita. Kutamanisha zaidi, ilikuwa nambari yake ya usajili KBR 001Z. “Bonge la wallpaper” alisikika mmoja akishangaa ndani ya basi.
Kushoto, palinguruma gari nyingine aina ya Hummer, almaarufu ‘nyundo’. huyu pia ni Ibilisi mwingine katika orodha ya maadui wa petroli. Nikimwita kifaru wa jiji hutanipinga. Maumbile yake, pamoja nasifa yake ya kutembea kifua mbele inalingana na ubingwa wake.
Mbele alirembeshwa kwa vyuma vya kumetameta. Nyuma alikosa nambari ya usajili hata tukashuku bado mgeni nchini. Kitendawili kumhusu ni uhusiano wake kimapenzi na wanasiasa nchini Kenya.ukitaka umaarufu huna budi kumchombeza.
Kwenye msafara, alifanya magari mengine ya kibinafsi kuonekana kama siafu. sitataja kina kaka Vitz, Alex,Runx, March, Probox orodha ni ndefu taja zingine........
Tuwache hayo. kuna huyu dereva wa vitz aliyeonekana kuwa na haraka na hata akapenyeza kijigari lake kwenye njia ya mguu kando kando hata kuwaudhi wapita njia. utanikashifu kwa kuwa mmbea lakini heri nimfichue.
Hayawi hayawi, hatimaye huwa. Polisi wa trafiki mwenye kitumbo cha kiriba alifungulia magari na taratibu msafara wa magari ulisonga kama jinsi mkondo wa mto huteremka mlima. Ghafla, mkondo ulishika kasi na magari yakapepea kwenye barabara kuu ya mbagathi.
Tulipofikia makutano ya barabara ya Langata, tulipata pamefanyika ajali mbaya sana. Kulingana na mashahidi wa karibu, dereva wa gari hilo aina ya Toyota Caldina alisemekana kupoteza mwelekeo kabla ya kurukia gomba la ndizi kando ya barabara. Gari ilijikunja sura ungedhani imepiga busu domo la gari moshi. "Wololo! Maskini!" alishangaa dereva wa basi.
Comments