Skip to main content

FEDHEHA ZA SWALEH

MTUNZI: MARIA REHEMA

Swaleh kijana wa miaka ishirini na tisa alienda usingizini, akiwaza na kuwazua jinsi atakavyo jishindia jiko. Alihesabu miaka yake na kustaajabu kuwa miaka hiyo yote, alikuwa anavunda upweke. Kisa na maana hakuwa na bila barafu wa roho.

Liwike lisiwike kutakucha. Swaleh aliamka na kabla ya kupata staftahi, alianza siku kwa kujipodoa. Liche ya uzito wake na kipipa cha tumbo, aliamua kuvaa shati na suruale iliyombana kupindukia. “ Ndo mavazi ya kisasa haya, nitaweza kuwapata warembo kadhaa,” alijiambia Swaleh.

Baada ya staftahi, Swaleh huyo kiguu na njia jijini kutafuta kipenzi cha roho. Bak bandika bak bandua mpaka kwenye kituo cha basi. Alipoingia kwenye ‘matatu’ moja akakutana na kidosho aliyerembeka mno.

Hakupoteza wakati alikimbia na kuketi karibu na mrembo huyo. Alivutiwa na macho yake makubwa yaliyong’aa na ngozi yake nyororo. Mwili wake je? Nikisema zaidi utamwonea wivu. Maumbile haya yalimtia Swaleh wazimu.

Bila shaka Swaleh alibaki mdomo wazi maneno yakimganda kinywani. Dakika kumi zilipita kama bado wawili hao hawajaongea. Swaleh alikuwa akimeza mate tu huku akimrushia kijicho cha tamaa. Matatu lilipofika jijini wawili hawa walishuka.

Msichana huyo aliposhuka aliangusha mkoba wake. Swaleh huyooo! Alitaka kuonyesha hisani na kwa hivyo hakusita kutoa msaad.

Alipoinama kuuchukua mfuko huo, ghafla! suruali yake iliraruka huko nyuma asijue la kufanya. ikiwa ulisoma jiografia utakumbuka chimbuko la bonde la ufa.  Hayo kando, mara Swaleh aliamka mbio kujiangalia huku haya ikimvaa usoni. Watu walioshuhudia tukio hilo hawangejizuia kicheko.


Kama kusugua chumvi kwenye kidonda, mara  kifungo cha suruali ya Swaleh iling’oka na kuruka kumwahi mwanamke mkongwe aliyekuwa katika umati uliomzingira. Swaleh aliinama ili kuzuia suruali yake kumvuka. Lakini aibu haijui be wala te, suruali iliraruka zaidi. 

Alichana mbuga na kuiingia na kuingia katika “ Public toilet”. Baada ya aibu hiyo, alijihisi kuenda msalani. Majasho yalikuwa yamemtoka midhili ya maji mferejini. Alipomaliza kujisaidia alienda kunawa mikono. Punde tu, alipofunguwa mfereji, maji yakatoka na fujo kumtoteshea upande wote wa mbele ya suruale yake.
 “Salala! Aibu gani hii, si nguo zangu kuraruka, sasa nimetota.” Swaleh alilia.

Alipokuwa njiani kwenda kwake, kila aliyempita Swaleh angedhania amejikojolea. Alipofika nyumbani kwake, aliufunga mlango wake na kufuli na kuketi chini. Alitafakari jinsi tamaa yake ya kupata mke ilivyomletea aibu mno. 

Usiku ulipofika, alijisongea sima na kukaanga mboga na akala. Alipokula, aliingia chumbani na kupanda kitandani akingoja usingizi umchukue. 
… katika kipindi kijayo cha Fedheha za Swaleh. 
“ Mwanangu huji kumtembelea mamako siku hizi?” Swabaha alilia.

Comments

Popular posts from this blog

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

MAPENZI KIZUNGU ZUNGU

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Mawimbi makali baharini yalikimbizana na hatimaye kusukuma maji hadi ufukweni. Pembeni, Bahati alionekana ameshika kijiti kirefu mkononi akijaribu kuchora umbo la moyo wa mapenzi kwenye changarawe mbichi huku maji ya bahari yakifuta. Angani, ndege aina ya korongo na mbayu wayu wangeonekana wakicheza cheza huku tufani kali zikifanya matawi ya minazi ufuoni kupukutika. Nikijistiri juu ya roshani(balcony) katika hoteli ambayo tulikuwa tumekodisha nilisalia kula kwa macho. Nilibakia kinywa wazi kuona madhari ya kutamanisha jinsi jua ilizama upeoni na kufanya maji ya bahari kupiga rangi ya manjano. mawazoni, nilitawaliwa na picha za harusi yetu jana yake katika ukumbi wa pataneni . Hatua chache niliona suti yangu ambayo ilikuwa ingali sakafuni baada ya usiku yenye sarakasi si kidogo. Ajabu, marashi yenye uhai aliyopiga Bahati ilikuwa bado imesakama pua yangu.Waliosema harusi ni kilele cha mapenzi hawakukosea hata kidogo. “Honey…………Rashidy! Rashidy!” Kwa...

SIRI ZA “JAM” JIJINI NAIROBI; TOLEO LA PILI

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Jinsi basi lilivyozidi kufukuzia kuelekea mzunguko wa Nyayo stadium, ndivyo ilizidi kuwachilia moshi ya mpingo iliyosokota angani kabla ya kutawanyika. Pale pia, tulimpata polisi wa trafiki mwanamke aliyefungia mshipi wa longi yake kwenye kifua. Amini usiamini, kwa ishara ya mkono alielekeza mkondo wa gari kama jinsi upepo huele ... keza bendera. Pale tulis...imama kwa dakika chache kabla ya msongamano kufunguliwa. Cha kuvutia tamaa ya macho yangu ilikuwa ‘tuk tuk’ fulani ambayo ilipenya penya kati kati ya magari huku ikipiga kelele kama mashine ya kusaga mahindi. Wenzangu wanaiita kule bara POSHOMILL. “We! Boss, ondoa hiyo kabati kwenye barabara” alisikika akishambuliwa na mmoja wa madereva wa matatu. Wanasema muungwana hununa moyoni na wala siyo mashavuni na kwa hivyo Yule dereva wa ‘tuk tuk’ akaridhia kumjibu kwa kimya. Kando na tukio hili, kuna jambo lililotendeka ambalo liliwacha mbavu za kila mtu zikiuma. Niseme nisiseme! Aaaah! ...