Skip to main content

BIBI WA KUTAFUTIWA!

Kwa Bi Saida
S.L.P 248
DAYSTAR, Athi-River
24/03/2011

Mama,
Habari za siku nyingi? Hivi naamini u salama wasalmin hata ikiwa utasema nmenyamaza sana. Kabla sijaendelea, ningependa kuuliza ikiwa ulipata gora ya leso niliyokutumia. Hata hivyo,Kama ulipata ni sawa.

Mama! Lengo na madhumuni ya kuiandika barua hii ni kulalama kuhusu binti mliyenitafutia. Naamini nyina hawezi kumpa mwanawe sumu. Lakini, ni wazi tunda ulilonichagulia kumbe ilivutia kwa nje ilhali ndani imeoza.

Sitaki nikupandishe presha bure, lakini, ni vema nikufichulie dosari zake kabla maji hayajazidi unga. Mama! Kitanda cha kifahari nimenunua lakini amini usiamini nimelala kila kukicha nikijishika tama. Kisa na maana, bibi ni mwana riadha wa usiku.

Kabla nifikie kuiandika barua hii. Nimetafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa kila aina. Lakini, tiba imeshindikana. Nimechoka kulipa dhamana ya kumkomboa kila anapotiwa nguvuni na askari wa baraza la jiji kwa shtaka la kukimbia ovyo usiku.

Hivi nikizungumza, tayari nishamweka kwenye basi ya kurudi alikotoka. Heri nijichagulie bibi hata kam nitaenda kinyume na na itikadi zetu.

Najuta ni kwanini nikakubali kauli yenu ya kumfukuza mpenzi wangu njoki kwa madai kwamba ni wa kabila tofauti.

Mama! najua umeudhika kwa vile nimepinga kauli yenu. Kumbuka ulinieleza kwamba mwana akinyelea paja halikatwi bali hupanguswa.

Nitakuja nyumbani jumapili ijayo tupate kujadiliana zaidi.

Mimi Mwanao
Radhia Onyango

Comments

nimo wa wambui said…
at first i thought mwanariadha wa usiku??????? wa wa hii iko juu
my say my take said…
nyc stuff keep it up i lyk it
@Nimo na Annabel shukran sana kwa mchango wenu katika ukurasa huu bila ya nyinyi hapa patakosa ladha. waalikeni wenzenu.

thanks! thanks! thanks!

Popular posts from this blog

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

OPERATION TUTETEE WANAUME!!!

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL SEHEMU YA KWANZA: Mzee Matendechere alionekana kuokotwa na usingizi mwepesi wakati akiuguza majeraha ya panga hospitalini. Kisa na maana, adabu ilimhama mkewe hata akaamua kuchukua sheria mkononi na kumpa mumewe kichapo cha mbwa kabla ya kutorokea kusichojulikana. Kichwa chake kilibanwa kwa kilemba cheupe chenye matone ya dam u. Isitoshe, Kwenye shavu la kushoto, palidhihirika jeraha bichi lenye kushonwa kwa uzi. Cha kusikitisha zaidi, Pembezoni mwa kitanda, wangeonekana wapiga picha kutoka vyumba vya habari waking’ang’ana kuchukua picha za kuvutia watazamaji. picha kwa hisani ya http://medievalminds.com Maskini Matendechere alizidiwa na usingizi hata akabakia kukoroma huku akifungua mdomo mithili ya mamba mwenye njaa. “Wow! This seems to be the best shot, I,m loving this” alisikika akisema mmoja wa wapigaji picha tuliyeshuku ni wa asili ya kimarekani. Kweli, vita vya panzi furaha ya kunguru. Wakati haya yakijiri, ndoto ya m...

KUMBU KUMBU ZA MWANA HAWA

MTUNZI: Odhiambo Danyell Manyunyu mepesi ya mvua yangesikika yakikung’uta mabati na kuibua mdundo flani iliozidisha tamaa yangu ya  kuendelea kupanga mbavu kwenye kitanda. Mara, alisikika jogoo mmoja kijijini akiwika kama kuashiria nuru ilikuwa imekubali zamu yake ya mchana. Nilibaki kugaragara kitandani huku mabishano makali yakiendelea akilini kati ya mwili dhaifu na nafsi yangu. Mwili ilisisitiza niendelee kulala huku nafsi ikinisihi niamke. Baada ya kutafakari kuhusu hasara za usingizi niliridhia kuamka. Ghafla, fikra zangu zilielekezwa katika saa kubwa iliyoning'inia ukutani ambayo ilikatiza hali ya unyamafu uliokuwa umetawala chumbani. kuzidisha, chenene fulani aliyekuwa kajificha mvunguni alianza kutoa sauti ya kuudhi. “Aah! Heri tuu niamke” nilijisemeza huku nikijikokota kuelekea kwenye dirisha. Nikichungulia nje, ningeona kunguru wakipigania makombo ya chakula kwenye pipa iliyosimama mkabala na chumba changu. Isitoshe, rukwama kukuu za wazegaz...