Skip to main content

Posts

KIVULI KIZITO CHA KIWEWE

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Wa kwanza alikuwa Rehema, njia zetu zilikutana kwenye ufuo wa bahari hindi msimu wa upanzi wa mwaka 1999. Kidonda hicho kingali kibichi. Japo nilibaki na kovu, nahisi ni kama nazungumzia ya jana. Kwa ufupi, yake na yangu yalikuwa mafupi hata ingawa vioja vilikuwa teletele. Uhusiano wa kunoga tulilinda kwa takriban miezi miwili. Siku moja, aliamka na kuniambia yu mja mzito. Nilimshauri akakiangamize kijusi hicho. Hii ilitokana na wingi wa uoga kuhusu majukumu ambayo yangendamana na hali hiyo. Alikubali wito japo shingo upande. Baadaye, niliarifiwa yuko hali mahututi katika katika zahanati ya Dr. Tiba wa Maradhi. Kesho yake Jioni , nilipata simu ya dharura. “harakisha mpenzio amevuja damu nyingi sana akijaribu kuavya mimba changa. Nasikitika kusema, si wa dunia hii tena.” hitimisho likawa ni maombolezi na baadaye mazishi huku vidole zote nikielekezewa. Vivyo hivyo, aliyefuatilia mkondo huu alikuwa kipusa kwa jina Amina. Mtoto yatima ambaye nilipata kum...
Recent posts

WENYEJI WA ZIWA BARINGO WANAUA UTALII................

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL CHUO KIKUU CHA DAYSTAR NAIROBI Magurudumu ya matatu yalikimbizana kuelekea kwenye lango kuu la ziwa Baringo. Nyuma yetu barabara ilikuwa safi japo kwa vumbi nyepesi pamoja na moshi ambayo ilionekana kutuandama kabla ya kusokota angani. Pembeni mwa lango hilo, palisimama wima kibao “Welcome to Lake Baringo” hii ikawa ni ridhisho tosha kwamba makaribisho kabambe yalikuwa yatungoja. Kama ada, tuliegesha gari mbele ya kizuizi cha baraza la jiji. yaliyofuata, yakawa ni kuhesabiwa kisha kulipia kiingilio. “Karibuni na mjienjoy kabisa” askari kwenye lango alitueleza. Baadaye, kizuizi kiliinuliwa kuashiria tulikuwa huru kuvinjari kila kona ya ziwa ambalo nilikuwa nimesikia tuu kupitia uvumi wa marafiki pamoja na maarifa ya vitabu za jiografia. Kuonekana kwa ziwa upeoni kuliwafanya hata waliokuwa wanasinzia kupata sababu ya kuchangamka. “Lake Baringo here we come!” kidosho aliyekuwa kando yangu alisema wakati akingangana kupiga picha kutumia si...

KUFUNGWA KWA SOKO YA BURMA NI FURAHA WAKAAZI WA NAIROBI

Mtunzi: Odhiambo Danyell Ni bayana kwamba wenyeji wa Nairobi na vitongoji vyake wana kila sababu ya kutabasamu baada ya tangazo la kufungwa kwa soko maarufu la nyama kwa jina Burma. Hatua hii imechochewa na  tabia ya  wafanyi biashara kukaidi kutii sheria za wakaguzi wa afya. Kabla ya kungamua hatari inayowakodolea macho walamba minofu katika soko hilo ni heri nikufafanulie taswira halisi angalau ufahamu chimbuko la  hatua hii. Punde tuu unapofika katika lango kuu la soko hilo utakaribishwa na harufu mbaya inayoninginia hewani. Kando na hayo, utashuhudia jaa kubwa la taka la kusheheni pembe za wanyama, makombo ya minofu pamoja na maji taka iliyozagaa kila sehemu. Hatimaye, utawaona chokora wakibishana na mbwa ambao hukukwangura jaa hilo wakitafuta pato lao. Kuingia ndani, utapishana na wafanyi biashara wa nyama waliovalia ovaroli chafu za kutona damu wakibeba bidhaa hiyo kiholela huku wakivuka mitaro iliyosakamwa na maji taka iliyoga...

OPERATION TUTETEE WANAUME!!!

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL SEHEMU YA KWANZA: Mzee Matendechere alionekana kuokotwa na usingizi mwepesi wakati akiuguza majeraha ya panga hospitalini. Kisa na maana, adabu ilimhama mkewe hata akaamua kuchukua sheria mkononi na kumpa mumewe kichapo cha mbwa kabla ya kutorokea kusichojulikana. Kichwa chake kilibanwa kwa kilemba cheupe chenye matone ya dam u. Isitoshe, Kwenye shavu la kushoto, palidhihirika jeraha bichi lenye kushonwa kwa uzi. Cha kusikitisha zaidi, Pembezoni mwa kitanda, wangeonekana wapiga picha kutoka vyumba vya habari waking’ang’ana kuchukua picha za kuvutia watazamaji. picha kwa hisani ya http://medievalminds.com Maskini Matendechere alizidiwa na usingizi hata akabakia kukoroma huku akifungua mdomo mithili ya mamba mwenye njaa. “Wow! This seems to be the best shot, I,m loving this” alisikika akisema mmoja wa wapigaji picha tuliyeshuku ni wa asili ya kimarekani. Kweli, vita vya panzi furaha ya kunguru. Wakati haya yakijiri, ndoto ya m...

SIRI ZA “JAM” JIJINI NAIROBI; TOLEO LA PILI

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Jinsi basi lilivyozidi kufukuzia kuelekea mzunguko wa Nyayo stadium, ndivyo ilizidi kuwachilia moshi ya mpingo iliyosokota angani kabla ya kutawanyika. Pale pia, tulimpata polisi wa trafiki mwanamke aliyefungia mshipi wa longi yake kwenye kifua. Amini usiamini, kwa ishara ya mkono alielekeza mkondo wa gari kama jinsi upepo huele ... keza bendera. Pale tulis...imama kwa dakika chache kabla ya msongamano kufunguliwa. Cha kuvutia tamaa ya macho yangu ilikuwa ‘tuk tuk’ fulani ambayo ilipenya penya kati kati ya magari huku ikipiga kelele kama mashine ya kusaga mahindi. Wenzangu wanaiita kule bara POSHOMILL. “We! Boss, ondoa hiyo kabati kwenye barabara” alisikika akishambuliwa na mmoja wa madereva wa matatu. Wanasema muungwana hununa moyoni na wala siyo mashavuni na kwa hivyo Yule dereva wa ‘tuk tuk’ akaridhia kumjibu kwa kimya. Kando na tukio hili, kuna jambo lililotendeka ambalo liliwacha mbavu za kila mtu zikiuma. Niseme nisiseme! Aaaah! ...

SIRI ZA 'JAM' JIJINI NAIROBI

MTUNZI:ODHIAMBO DANYELL Dereva wa basi la kampuni ya RWAKEN alijistiri mbele ya usukani na kupiga gari moto wakati tukiondoka katika kitivo cha chuo kikuu cha Daystar yenye makao katika mzunguko wa barabara ya Valley road, Nairobi. Il ikuwa dakika chache baada ya saa kumi na nusu jioni. Hii ni kumaanisha, wafanyikazi pamoja na wanafunzi wa mchana chuoni tayari walikuwa katika harakati zakufunganya virago na kurejea makwao baada ya panda shuka za mchana. Vvrrrrrrrrrrrrrm! vvrrrrrrrm! Dereva alipasha gari moto na taratibu basi likaelekezwa nje ya lango kuu. kabla ya kuingia kwenye barabara kuu ya Valley road. Auuuuuwi! imagine mbele yetu palisimama gari aina ya Range Rover Vogue iliyowachilia moshi nyeupe iliyosokota na kupata hifadhi katika mapua ya basi la RWAKEN. Katika mbuga la wanyama, gari hili linalinganishwa na mfalme Simba kutokana na udhabiti wake. Mashini hii yasifika kwa ulafi wa petroli pamoja na muundo wake wa kutamanisha. Aha! Sasa nimejua kwanini basi ilikuw...