Skip to main content

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo

Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta.

Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili.

Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya.

Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi.

Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa.

Mahuluku taabu nawafananisha na mshale wa kuhesabia sekunde kwa maana, wao hufanya kazi zaidi hata ingawa maumbile yao yameshiba unyonge. Kama tuu mshale wa sekunde, wenyeji katika kiwango hiki hulazimishwa kulipa kodi hata ingawa kipato ni kilegevu.

Ukihesabu, utagundua kwamba mshale wa sekunde huzunguka mara elfu moja mianne na arobaini kila siku. Si bure, wakenya hawa huandamana kila mara kutokana na unyanyasaji unaofanywa dhidi yao.

Kwingineko, mshale wa kadri ama ukipenda wa kurekodi dakika unalingana na wakenya wa maisha ya wastani. Kiwango hiki chajumlisha wale walomudu kupata elimu na hatimaye wakabahatika kuhifadhi nafasi za katikati serikalini na katika kampuni za kibinafsi.

Hapa, kazi ni kiasi na kipato ni kiasi ndo maana mshale wa dakika huzunguka mara ishirini na nne pekee kwa siku . hebu tafakari tofauti kubwa iliyoko ikilingana na kazi ya mshale ya sekunde.

Mwishowe, kuna ile mshale wa kuhesabu masaa. Kimatani anaitwa “hatunganani ila twavuma” bwana huyu anasifika kwa unyanyasaji dhidi ya wenzake. Hata ingawa huzunguka mara mbili tuu kwa siku, yeye ndiye mwenye ushawishi zaidi.

Kimaumbile, yeye ni mfupi na kibonge. Isitoshe, itakubidi ukaze macho zaidi ili kumwona akitekeleza wajibu wake. Katika Kenya yetu, mshale huu unafananishwa na viongozi wetu ambao kazi yao imekua ni kupayuka na kutoa ahadi za uwongo huku wakizidi kufilisi mlipa kodi.

Hebu sasa tazama viwango tofauti katika jamii ukilinganisha na mishale hizi za saa. Kazi ya wanasiasa pamoja na wale wa kipato cha wastani kamwe haiwezi kulinganishwa na jasho ya wakenya wanaopata malipo ya chini ya dola kwa siku.

Jee! Itakuwaje siku moja mshale ya kuhesabu sekunde ikisusia kazi? Hata labda hii ndoo maana ya wewe kuchelewa kwenda darasani ama kazini leo asubuhi.

Comments

Unknown said…
Interesting perspective,,very interesting.

Popular posts from this blog

OPERATION TUTETEE WANAUME!!!

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL SEHEMU YA KWANZA: Mzee Matendechere alionekana kuokotwa na usingizi mwepesi wakati akiuguza majeraha ya panga hospitalini. Kisa na maana, adabu ilimhama mkewe hata akaamua kuchukua sheria mkononi na kumpa mumewe kichapo cha mbwa kabla ya kutorokea kusichojulikana. Kichwa chake kilibanwa kwa kilemba cheupe chenye matone ya dam u. Isitoshe, Kwenye shavu la kushoto, palidhihirika jeraha bichi lenye kushonwa kwa uzi. Cha kusikitisha zaidi, Pembezoni mwa kitanda, wangeonekana wapiga picha kutoka vyumba vya habari waking’ang’ana kuchukua picha za kuvutia watazamaji. picha kwa hisani ya http://medievalminds.com Maskini Matendechere alizidiwa na usingizi hata akabakia kukoroma huku akifungua mdomo mithili ya mamba mwenye njaa. “Wow! This seems to be the best shot, I,m loving this” alisikika akisema mmoja wa wapigaji picha tuliyeshuku ni wa asili ya kimarekani. Kweli, vita vya panzi furaha ya kunguru. Wakati haya yakijiri, ndoto ya m...

KUMBU KUMBU ZA MWANA HAWA

MTUNZI: Odhiambo Danyell Manyunyu mepesi ya mvua yangesikika yakikung’uta mabati na kuibua mdundo flani iliozidisha tamaa yangu ya  kuendelea kupanga mbavu kwenye kitanda. Mara, alisikika jogoo mmoja kijijini akiwika kama kuashiria nuru ilikuwa imekubali zamu yake ya mchana. Nilibaki kugaragara kitandani huku mabishano makali yakiendelea akilini kati ya mwili dhaifu na nafsi yangu. Mwili ilisisitiza niendelee kulala huku nafsi ikinisihi niamke. Baada ya kutafakari kuhusu hasara za usingizi niliridhia kuamka. Ghafla, fikra zangu zilielekezwa katika saa kubwa iliyoning'inia ukutani ambayo ilikatiza hali ya unyamafu uliokuwa umetawala chumbani. kuzidisha, chenene fulani aliyekuwa kajificha mvunguni alianza kutoa sauti ya kuudhi. “Aah! Heri tuu niamke” nilijisemeza huku nikijikokota kuelekea kwenye dirisha. Nikichungulia nje, ningeona kunguru wakipigania makombo ya chakula kwenye pipa iliyosimama mkabala na chumba changu. Isitoshe, rukwama kukuu za wazegaz...