Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2011

SIRI ZA CHUO KIKUU CHA DAYSTAR

Njoo unisome kwa makini S.L.P 927 MACHO PLAZA Kwa wewe unayenisoma, Habari za utokako? Naona unahema kweli ukitaka kujua yaliyojiri hivi leo kwenye barua hii. Hee! By the way, ikiwa wataka tuelewane naomba uwache kuniangalia kwa hizo macho za kushiba chuki na dharau. Kabla nikuendelezee udaku! Tafadhali wacha kuangalia kando kando ukinisoma. Unawafanya wapita njia wanadhani tunawasengenya humu. By the way, usha ambiwa na yeyote hivi leo kwamba watamanisha? Ooooooooooooh! Nisamehe. I mean.... you are fearfully and wonderfully made. Sitaongeza wala sitapunguza. Niwie radhi siwes kutranslate, please! Mwelezee.. aliye kando yako aje akusaidie. Kabla nikupatie udaku, natamani niulize swali moja tuu. Nihakikishie kwamba hutanuna! Naogopa lakini heri niulize tuu atleast tusafiane nia. Hivi mbona una blush sana? Kama nimekubamba si uniambie tuu ama uwaite wanafunzi wenzako waje wasome uhondo. Matawi ya miti naona inapukutika kutokana na upepo mkali unaofagilia kutoka milima ya l...

MAPENZI KIZUNGU ZUNGU “SEASON TWO”

“Darling funga macho nikuambie kitu” Bahati alinishurutisha kwa sauti ya upole. Bila kusita, nilifikicha macho yangu kwa viganja vya mkono nikiwa na hamu ya kujua kilichokuwa chaningoja. Bahati alikuwa na uzoefu wa kunifanyia utani wa aina hii haswa wakati penzi lilkuwa limemchachawiza. Mara ya mwisho alitumia mbinu hii, ni wakati aliponiletea pete ya dhahabu afisini. Wakati nilipokuwa nimeziba macho, mawazo mengi yaligongana akilini. “labda ana siri Fulani anataka kunieleza ama ni zawadi anataka kunipa? aaah! Potelea mbali, liwe liwalo!” nilijisemeza moyoni. Ghafla, Mlipuko mkubwa ulisikika hatua chache. sekunde kadhaa baadaye, nilijipata nimelala kifudifudi ardhini huku shati yangu ikitoja damu. “Mungu wangu! Mungu wangu! ” nilibaki kupiga kite huku nikichirizikwa ovyo na damu utosini. Nilikazana kulinda nguvu kiasi niliyokuwa nimebaki nayo, macho yangu yalipepesa na kuranda randa ovyo nikitafuta alipokuwa Bahati wangu. Mita chache, niliona mawimbi ya bahari yenye hasira y...

KUAGA KWA GWIJI, MJ

Dunia iliomboleza, kulala kwa Gwiji MJ tulimpoteza, vilio kwenye miji Mauti umetukaza, Na tukutane kwa jaji Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop Mauti huna arafa, tutayarishe mapema Robot densi ilifaa, moon walk ikavuma Ingawa ulikufa, sifa zitakusakama Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop Mahasidi wenye wivu, kakupeleka kizimba Wakakupa maumivu, bila hatia ukaimba Umerudi kuwa jivu, kwetu ungali simba Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop Mahala pema peponi, Na ilale roho yako Takulinda kama mboni, zisipotee sifa zako Sinayo woga usoni, kukupea wewe heko Kwaheri ya kuonana Mfalme wa Pop

MAPENZI KIZUNGU ZUNGU

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL Mawimbi makali baharini yalikimbizana na hatimaye kusukuma maji hadi ufukweni. Pembeni, Bahati alionekana ameshika kijiti kirefu mkononi akijaribu kuchora umbo la moyo wa mapenzi kwenye changarawe mbichi huku maji ya bahari yakifuta. Angani, ndege aina ya korongo na mbayu wayu wangeonekana wakicheza cheza huku tufani kali zikifanya matawi ya minazi ufuoni kupukutika. Nikijistiri juu ya roshani(balcony) katika hoteli ambayo tulikuwa tumekodisha nilisalia kula kwa macho. Nilibakia kinywa wazi kuona madhari ya kutamanisha jinsi jua ilizama upeoni na kufanya maji ya bahari kupiga rangi ya manjano. mawazoni, nilitawaliwa na picha za harusi yetu jana yake katika ukumbi wa pataneni . Hatua chache niliona suti yangu ambayo ilikuwa ingali sakafuni baada ya usiku yenye sarakasi si kidogo. Ajabu, marashi yenye uhai aliyopiga Bahati ilikuwa bado imesakama pua yangu.Waliosema harusi ni kilele cha mapenzi hawakukosea hata kidogo. “Honey…………Rashidy! Rashidy!” Kwa...