Skip to main content

Posts

Kwa mpenzi wangu Bi Omena.

Rashidy Mpendwa Kwa mpenzi wangu Bi Omena. Sanduku la posta 10, Jangwani. Lazizi, Mwaaaaah! ama wataka busu nyingine? Nimeandika barua hii kwa hofu kuu kwani naogopa hii ni mara ya mwisho tutakutana kwenye mji mkuu wa sahani. Amini usiamini, nitamisi sana tabia yako nzuri ya kunitengezea kitoweo cha kufinyanga kwa sima wa mahindi. Kwa hakika, sina furaha kwani ahadi zako kwamba tutakutana sokoni zimeambulia patupu.kila wakati nimeenda sokoni sijakupata. nimewapata tuu mandugu na madada zako kiboma, kambare, mbuta na tilapia. Shemeji yako Tilapia ameniarifu kwamba idadi ya familia yenu imepungua sana katika ziwa victoria. Kisa na maana,Tilapia aliteta vikali kwamba chemichemi ya maji ya mau imeharibiwa pakubwa na jamii ya wanadamu. ailisistiza kwamba msitu huo uhifadhiwe ikiwa nataka kuonja tena kitoweo chako. Mpenzi, wajua kwamba nakuota kila nikila? matonge ya sima yananinyonga kila nikiwaza kukuhusu. By the way nimeamua nitakujengea bonge la swimming pool uje uishi na fam...

MAKARIBISHO YA WANAFUNZI WAGENI CHUONI DAYSTAR!

Hayawi! Hayawi! Hatimaye huwa. Msafara mrefu wa magari ya kifahari ulitawala barabara kuu ya mchanga kuelekea katika lango kuu la chuo cha Daystar, Athiriver. Kwangu ilikuwa ni kama jonzi kwani maishani halikuwahi kunidara wazo kwamba siku ingenijia ya kujiunga na chuo hili maaarufu. Nikijisitiri kwenye piki piki moja kuu kuu ambayo ilinikumbusha kisa cha punda mzee aliye rusha mateke, kupiga nduru na kulia machozi alipofanyishwa kazi ya sulubu bila ya mwenyewe kujali.vivyo hivyo pikipiki ilisikika kuyumba yumba huku ikitoa sauti kubwa na moshi ya mpingo iliyosokota angani bila ya dereva kushtuka. Wakati mbwe mbwe na shamra shamra zikitawala tulipofikia msafara huo katika lango kuu chuoni humo sikuwachwa nyuma kwani niliwasili kwa ‘style’ya aina yake. Godoro niliifunga mgongoni, begi kubwa yenye picha kubwa ya "rambo" ikiniwekelea tako utosini na ndoo ikininginia taratibu begani. Zaidi, dereva wa pikipiki alitia nakshi taswira hii kwa kuwasili kwa kishindo kikubwa. A...