Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2012

WENYEJI WA ZIWA BARINGO WANAUA UTALII................

MTUNZI: ODHIAMBO DANYELL CHUO KIKUU CHA DAYSTAR NAIROBI Magurudumu ya matatu yalikimbizana kuelekea kwenye lango kuu la ziwa Baringo. Nyuma yetu barabara ilikuwa safi japo kwa vumbi nyepesi pamoja na moshi ambayo ilionekana kutuandama kabla ya kusokota angani. Pembeni mwa lango hilo, palisimama wima kibao “Welcome to Lake Baringo” hii ikawa ni ridhisho tosha kwamba makaribisho kabambe yalikuwa yatungoja. Kama ada, tuliegesha gari mbele ya kizuizi cha baraza la jiji. yaliyofuata, yakawa ni kuhesabiwa kisha kulipia kiingilio. “Karibuni na mjienjoy kabisa” askari kwenye lango alitueleza. Baadaye, kizuizi kiliinuliwa kuashiria tulikuwa huru kuvinjari kila kona ya ziwa ambalo nilikuwa nimesikia tuu kupitia uvumi wa marafiki pamoja na maarifa ya vitabu za jiografia. Kuonekana kwa ziwa upeoni kuliwafanya hata waliokuwa wanasinzia kupata sababu ya kuchangamka. “Lake Baringo here we come!” kidosho aliyekuwa kando yangu alisema wakati akingangana kupiga picha kutumia si...

KUFUNGWA KWA SOKO YA BURMA NI FURAHA WAKAAZI WA NAIROBI

Mtunzi: Odhiambo Danyell Ni bayana kwamba wenyeji wa Nairobi na vitongoji vyake wana kila sababu ya kutabasamu baada ya tangazo la kufungwa kwa soko maarufu la nyama kwa jina Burma. Hatua hii imechochewa na  tabia ya  wafanyi biashara kukaidi kutii sheria za wakaguzi wa afya. Kabla ya kungamua hatari inayowakodolea macho walamba minofu katika soko hilo ni heri nikufafanulie taswira halisi angalau ufahamu chimbuko la  hatua hii. Punde tuu unapofika katika lango kuu la soko hilo utakaribishwa na harufu mbaya inayoninginia hewani. Kando na hayo, utashuhudia jaa kubwa la taka la kusheheni pembe za wanyama, makombo ya minofu pamoja na maji taka iliyozagaa kila sehemu. Hatimaye, utawaona chokora wakibishana na mbwa ambao hukukwangura jaa hilo wakitafuta pato lao. Kuingia ndani, utapishana na wafanyi biashara wa nyama waliovalia ovaroli chafu za kutona damu wakibeba bidhaa hiyo kiholela huku wakivuka mitaro iliyosakamwa na maji taka iliyoga...