MTUNZI: MARIA REHEMA Swaleh kijana wa miaka ishirini na tisa alienda usingizini, akiwaza na kuwazua jinsi atakavyo jishindia jiko. Alihesabu miaka yake na kustaajabu kuwa miaka hiyo yote, alikuwa anavunda upweke. Kisa na maana hakuwa na bila barafu wa roho. Liwike lisiwike kutakucha. Swaleh aliamka na kabla ya kupata staftahi, alianza siku kwa kujipodoa. Liche ya uzito wake na kipipa cha tumbo, aliamua kuvaa shati na suruale iliyombana kupindukia. “ Ndo mavazi ya kisasa haya, nitaweza kuwapata warembo kadhaa,” alijiambia Swaleh. Baada ya staftahi, Swaleh huyo kiguu na njia jijini kutafuta kipenzi cha roho. Bak bandika bak bandua mpaka kwenye kituo cha basi. Alipoingia kwenye ‘matatu’ moja akakutana na kidosho aliyerembeka mno. Hakupoteza wakati alikimbia na kuketi karibu na mrembo huyo. Alivutiwa na macho yake makubwa yaliyong’aa na ngozi yake nyororo. Mwili wake je? Nikisema zaidi utamwonea wivu. Maumbile haya yalimtia Swaleh wazimu. Bila shaka Swaleh alibaki md...
JAMVI LA BURUDANI,MAARIFA NA USHAURI