Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2011

MAZINGAOMBWE YA SAA

Na Danyell Odhiambo Nimejirusha kwenye kiti kilegevu cha msonobari nikifikiria jinsi hali ya maisha nchini Kenya inavyozidi kupaa kila uchao. Mbele yangu, pametulia redio, kando pamesimama kikombe cha kahawa chungu na juu pananinginia saa ya ukuta. Ghafla, fikra zangu zinatekwa nyara na saa iliyozubaa ukutani. Nikiangazaangaza, naona imetimia usiku mkuu. Hii ni kumaanisha, mishale yote ya saa imekutana kifuani pa namba kumi na mbili. Ukipiga hesabu kwa makini, utakubalina nami kwamba tukio kama hili hujirudia mara mia tatu sitini na tano kila mwaka. Ukumbuke, kisa hiki pia huashiria kuzaliwa kwa siku mpya. Hata ingawa mishale hizi zimedhibitisha ushirikiano ni kiungo muhimu katika katika kikundi, taswira fulani inaibuka nikiangalia mishale hizo. Taswira yenyewe yahusu tabia mbovu ya wabunge kukaidi shinikizo za kuwataka kulipa malimbikizi yao ya kodi. Nikipamabanua kitendawili hiki, itakubali kwamba jamii imejigawanya kupitia mishale hizi tatu za saa. Mahuluku taabu nawafa...

KULIFANYIKA NINI KATIKA KONGAMANO LA AFYA NA MAENDELEO - SAFARI PARK

“Aisee! nani anashukia safari park?” Makanga wa matatu ya kuelekea Githurai alipaza sauti akiuliza. “Mimi hapa!” nilimjibu huku nikikazana kupenya katikati ya abiria. Hewani, palishiba midundo mizito ya mziki iliyosambazwa kupitia spika kubwa zilizostiriwa chini ya viti. “Hujaniregeshea change yangu!” nilimkabili makanga mlangoni. “Ulinipa pesa ngapi?” aliuliza akihema utadhani ni yeye amebeba gari kutoka mjini. Kuvutia zaidi, kijasho chembamba kilimtiririka njia mbili mbili mashavuni na kudondoka kwenye shati yake ya manjano. Kwa sekunde chache, nilizubaishwa na mavazi ya makanga yule wa kiwiliwili cha wastani. Kichwani alivalia kofia nyekundu ya kuchujuka rangi iliyonakshiwa na maandishi “kazi kwa vijana”.Kiwiliwili kilijificha ndani ya kabuti kubwa iliyomfanya afanane "hatari bin danger" Mashavuni palisongamana “msitu” ndevu zilizochakaa hata nikashuku ni makao wanyama pori. Taya (jaws) zake nazo zilichapa kazi ungedhani ni mtambo wa kusaga mahindi. Gololi za macho ...

BIBI WA KUTAFUTIWA!

Kwa Bi Saida S.L.P 248 DAYSTAR, Athi-River 24/03/2011 Mama, Habari za siku nyingi? Hivi naamini u salama wasalmin hata ikiwa utasema nmenyamaza sana. Kabla sijaendelea, ningependa kuuliza ikiwa ulipata gora ya leso niliyokutumia. Hata hivyo,Kama ulipata ni sawa. Mama! Lengo na madhumuni ya kuiandika barua hii ni kulalama kuhusu binti mliyenitafutia. Naamini nyina hawezi kumpa mwanawe sumu. Lakini, ni wazi tunda ulilonichagulia kumbe ilivutia kwa nje ilhali ndani imeoza. Sitaki nikupandishe presha bure, lakini, ni vema nikufichulie dosari zake kabla maji hayajazidi unga. Mama! Kitanda cha kifahari nimenunua lakini amini usiamini nimelala kila kukicha nikijishika tama. Kisa na maana, bibi ni mwana riadha wa usiku. Kabla nifikie kuiandika barua hii. Nimetafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa kila aina. Lakini, tiba imeshindikana. Nimechoka kulipa dhamana ya kumkomboa kila anapotiwa nguvuni na askari wa baraza la jiji kwa shtaka la kukimbia ovyo usiku. Hivi nikizungumza, tay...