Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2010

MAKARIBISHO YA WANAFUNZI WAGENI CHUONI DAYSTAR!

Hayawi! Hayawi! Hatimaye huwa. Msafara mrefu wa magari ya kifahari ulitawala barabara kuu ya mchanga kuelekea katika lango kuu la chuo cha Daystar, Athiriver. Kwangu ilikuwa ni kama jonzi kwani maishani halikuwahi kunidara wazo kwamba siku ingenijia ya kujiunga na chuo hili maaarufu. Nikijisitiri kwenye piki piki moja kuu kuu ambayo ilinikumbusha kisa cha punda mzee aliye rusha mateke, kupiga nduru na kulia machozi alipofanyishwa kazi ya sulubu bila ya mwenyewe kujali.vivyo hivyo pikipiki ilisikika kuyumba yumba huku ikitoa sauti kubwa na moshi ya mpingo iliyosokota angani bila ya dereva kushtuka. Wakati mbwe mbwe na shamra shamra zikitawala tulipofikia msafara huo katika lango kuu chuoni humo sikuwachwa nyuma kwani niliwasili kwa ‘style’ya aina yake. Godoro niliifunga mgongoni, begi kubwa yenye picha kubwa ya "rambo" ikiniwekelea tako utosini na ndoo ikininginia taratibu begani. Zaidi, dereva wa pikipiki alitia nakshi taswira hii kwa kuwasili kwa kishindo kikubwa. A...